Afisa wa Zamani wa Polisi Aliyetekeleza Mauaji Kuachiliwa Huru

Former Police Constable Dickson Munene and Aggrey Mbai, serving life imprisonment at Kamiti Maximum Prison, with Limuru East ward nominated MCA Mercy Nungar

Dickson Mwangi Munene, afisa wa zamani wa polisi hivi karibuni atatembea huru baada ya kukamatwa kwa madai ya kumpiga risasi mtoto wa mbunge wa zamani.

Munene alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua, James Ngang’a, mtoto wa mbunge wa zamani Patrick Muiruri.

Mwangi, alitoa ombi la kuhukumiwa tena kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu mnamo mwaka 2017. Afisa huyo wa zamani aliomba Mahakama ipitie tena kesi yake ya madai ya mauaji na wizi wa kimabavu.

 

Alexander Chepkonga (left), and Dickson Munene in Nairobi Court September 2014 where they were charged with the murder of Dr James Ng'ang'a Muiruri in Westlands

Korti, kwa hiyo, ilizingatia miaka 10 Munene aliitumikia katika gereza la Kamiti ambapo alielezewa kama mfungwa wa mfano.

Alisoma akiwa gerezani na kupata shahada ya Masters katika masomo ya biashara, ambayo ilimfanya kutambuliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza ambaye alimpa cheti cha kuwa mfungwa wa mfano.

Kupitia wakili wake, Kioko Kilukumi, Munene aliiambia korti hali ya maisha ya familia yake imezorota, haswa kwani yeye ndiye aliyekuwa tegemeo pekee na alikuwa gerezani.

Alifafanua pia kuwa alipatwa na shinikizo la damu kwa sababu ya hali ya gereza.

Wakili wa Munene pia aliiambia mahakama kuwa juhudi za kupatana na familia ya marehemu hazijafua dafu na kwamba alijuta kwa tukio lililosababisha kifo.

Image result for dickson mwangi munene

Mnamo Januari 24, 2009, alishtakiwa kwa mauaji ya Ng’ang’a huko Westlands. Marehemu alipigwa risasi na kuuawa mida ya saa moja asubuhi baada ya kuzozana na afisa huyo.

Ng’ang’a ambaye wakati huo alikuwa na miaka 29, alikuwa amemaliza kozi yake ya digrii ya PhD katika sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Sheffield huko Uingereza.

Munene na mwenzake Alexander Chepkonga walipatikana na hatia ya kumuua Ng’ang’a, hata hivyo, mwenzake Alexander alifanikiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo na akaachiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *