Masaibu zaidi kwa Waituti, Serikali Yampokonya Ardhi yenye Dhamani ya Milioni Ksh100

Serikali  Alhamisi, Septemba 26, ilikichukua kipande cha ardhi ambacho gavana wa Kiambu Ferdinard Waituti anatuhumiwa kumpa kiharamu Esther Nyatu.

Kulingana na Jarida la Daily Nation, gavana huyo anakabiliwa na mashtaka mapya ya matumizi mabaya ya mamlaka. Tume ya Sheria ya Tawala (CAJ) ilikirudisha kipande hicho cha ardhi chenye thamani ya shilingi milioni 100 na kumrudishia Cecilia Mbugua ambaye ni mjane.

Mwenyekiti wa CAJ, Florence Kajuju wakati akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi, alisema kuwa atakabidhi matokeo ya uchunguzi huo dhidi ya gavana kwa Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP).

“Tutawasilisha ripoti yetu kwa ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai. Hii ni kwa sababu Hatujaruhusiwi kushtaki. Tunafuata uchunguzi wetu na ikiwa tutampata na mashtaka ya kujibu tutawasilisha kwa idara husika. , “Bi Kajuju alisema.

Walakini, akizungumza na kenyans.co.ke, Waititu alihoji muda wa kesi zake nyingi na kulia ilikuwa njama ya kumuangamiza.

“Jiulize kwa nini kesi zote hizi na madai hayo yanatolewa kwa wakati huu? zimekuwa nyingi na mimi ndiye mwathirika.Nia yao kubwa ni kuchafua jina langu,” alisema.

Ardhi husika (iliyoko Thika) ilikuwa swala nzito tangu 2013 baada ya Mbugua kutafuta idhini ya kuiwekeza kutoka Serikali ya Kaunti ya Kiambu.

Ripoti za Daily Nation zilidai kwamba alipewa barua ya idhini ambayo ilibatilishwa baadaye kwa madai kwamba kilikuwa ni cha chama cha Jua Kali.

Mbugua aliendelea kudai kuwa alikuwa amealikwa kwenye ofisi ya Waititu na akaamuriwa kutoa viwanja viwili kati ya vitano alivyo navyo au hangepata idhini aliyokuwa akitafuta.

Waititu anashutumiwa kubadilisha umiliki wa ardhi hiyo na kumpa Nyatu mnamo Januari 2018, bila makubaliano yoyote ya kuuza au malipo yoyote ya benki kuhalalisha mabadiliko ya umiliki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *