Alshaabab Watekeleza Shambulizi lingine, Idadi ya Watu Waliofariki Yahofiwa kuwa Kubwa

Wanamgambo wa Al-Shabaab wametekeleza shambulizi lingine katika nchi jirani ya Somalia, kisa kiki kimetokea siku mbili tu baada ya shambulio lingine kutekelezwa kwenye kambi ya jeshi karibu na Mogadishu.

Katika shambulizi lililotekelezwa alfajiri, Alhamisi katika kambi wa jeshi ya Abdalla Birole watu kadhaa kati yao raia na vikosi vya Jubaland wanahofiwa kupoteza maisha yao.

Shambulio hilo lilitokea karibu na mji  wa bandari ya Kismayo, ambayo kwa kiasi kikubwa iko chini ya ulinzi wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya chini AMISOM.

Serikali ya jimbo la Jubaland bado haijathibitisha rasmi shambulizi la hivi karibuni dhidi ya vikosi vya usalama. Jubaland ni mojawapo wa jimbo tulivu nchini somalia

“Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kutekeleza  mashambulizi dhidi ya jeshi la Jubaland huko Abdalla Birole, nje ya mji wa Kismayo, kusini mwa Somalia,” ripoti ilisema.

Shambulizi hilo linakuja wakati uhusiano kati ya kiongozi wa Jubaland Ahmed Madobe na Rais Mohammed Farmaajo inapitia wakati mgumu.

Madobe alichaguliwa mnamo agosti katika uchaguzi uliojaa utata. Uchaguzi huo uliungwa mkono na jeshi la Kenya lakini ukapingwa na Serikali kuu ya Somalia. Hata hivyo, Madobe alisitisha uapisho wake uliotarajia kufanyika Alhamisi, Uamuzi uliochochewa na kusitishwa kwa safari za ndege zilizoelekea uwanja wa kismayo.

Sio mara ya kwanza wanamgambo kushambulia kambi ya jeshi. Mnamo mwaka wa 2016, wanajeshi zaidi ya 200 wa KDF waliuawa El Adde. Mwaka mmoja baadaye, KDF ilipoteza askari zaidi ya 70 katika shambulizi lingine huko Kulbiyow.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *