Murgor aripoti Vitisho kwa Polisi, Ataka uchunguzi Ufanywe

Lawyers Philip Murgor and Cliff Ombeta at a press conference

Wakili wa Sarah Wairimu Philip Murgor amemtuhumu aliyekuwa mbunge wa Gatundu Kaskazini Patrick Muiruri kwa kumtishia wakati wa mazishi ya Tob Cohen Jumanne.

Katika barua iliyoandikwa Septemba 25 ikielekezewa mkuu wa kituo cha polisi cha Parklands, Murgor alisema Muiruri alitishia kukabiliana naye baada ya Murgor kumtaka binti ya muiruri asongebali na kaburi la wayahudi.

“Hapo awali kwa maagizo kutoka kwa mteja wangu, nilimuuliza kwa heshima binti ya Muiruri kuondoka kaburini kwani mazishi yalikuwa ibada ya kibinafsi ya familia tu,” Murgor alisema.

Muiruri alikuwa rafiki wa karibu wa Cohen. Murgor alisema mbunge huyo wa zamani alimtukana.

“Baada ya hapo, akanidharau na kunifokea: ‘Nitashughulikia wewe kule nje’. Aliponisogelea, alizuiliwa na Bw Chege Kirundi na Bw Cliff Ombeta – mawakili ambao kwa bahati nzuri walikuwa karibu. Tukio hilo lilishuhudiwa na wakili George Ouma,” Murgor alisema.

“Nachukulia tukio hili kama tishio na jaribo la kuniogopesha mimi kama wakili wa Bi Cohen. Kwa hivyo, nimeamua kuwasilisha malalamiko kwako rasmi na kukuhimiza uanzishe uchunguzi kuhusu dhamira za vitisho hivyo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *