Vifurushi 77 vya pedi vyapatikana shuleni ambapo msichana alijiua baada ya kuabishwa: Ripoti

Period shame girl bomet

Maelezo mapya yameibuka kuhusu wakati wa mwisho wa msichana wa Bomet ambaye alijiua baada ya kudaiwa kudharauliwa na mwalimu wake juu ya damu ya hedhi.

Katika ripoti ya awali ya Tume ya Huduma ya Walimu (TSC), imebainika kuwa Jackline Chepngeno alipata aibu shuleni, ambayo ilimwongoza kujiua, haya yakifanyika, taulo za hedhi zilikuwa katika ofisi ya naibu mkuu na nyumbani kwake.

Mnamo Septemba 6, siku ambayo alijitia kitanzi, kulikuwa na pakiti 77 za taulo za usafi kwenye duka la Shule ya Msingi ya Kabiangek huko Konoin, Bomet.

“Shule hiyo ilikuwa imepokea taulo kamili za usafi kwa muhula wa pili,” ripoti iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSC Nancy Macharia ilisoma kwa sehemu.

Akiwa nyumbani, Jackline alikuwa ameiachia pakiti moja kwenye sanduku lake, kulingana na ripoti ya ukurasa wa 42 iliyowasilishwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Bunge ya elimu Alhamisi.

Bildergebnis für bomet girl

Mwanafunzi huyo alikuwa ni mmoja wa wasichana 50 ambao walikuwa wakipokea vifaa vyao vya usafi kutoka shule yao mnamo Julai. Kila moja yao alikabidhiwa na pakiti mbili za matumizi wakati wa mwezi wa Agosti na Septemba.

Mama wa Jackline, Beatrice Kirui, alithibitisha kwa timu ya uchunguzi iliyoongozwa na mkurugenzi wa elimu wa Kaunti ya Bomet kuwa msichana huyo alikuwa na pakiti moja ya pedi ambazo hazijatumiwa.

Taarifa ya Bi Kirui, hata hivyo, inapingana na taarifa iliyorekodiwa na mwalimu huyo, ambaye alikuwa mwalimu wa darasa la Jackline na kumfundisha Kiingereza.

Katika taarifa yake, Bi Chemutai alisema hakumdharau wala kumpeleka mwanafunzi huyo nyumbani wakati wachunguzi wakidai alizungumza na msichana “kwa heshima”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *