Polisi Waamuriwa kumpa Sossion Ulinzi Afisini Mwake

Knut secretary general Wilson Sossion and chairman Wycliffe Omuchayi at their office in Nairobi.

Kamanda wa polisi wa kaunti Ijumaa alielekezwa kuhakikisha kwamba katibu mkuu wa Knut anayegomewa Wilson Sossion anafika salama salimini ofisi yake kaika Mtaa wa Mfangano, Nairobi.

Kamanda na Afisa wa kituo cha polisi cha Kamukunji wameamuriwa kumhakishia usalama madhubuti  .

Jaji wa Ajira na Uhusiano wa Ajira Maureen Onyango alitoa agizo hilo kufuatia agizo la Jaji Hellen Wasilwa la tarehe 2 Septemba ambalo lilimrejesha Sossion kama bosi wa muungano huo hadi kesi aliyowakilisha itakapoamuriwa.

Sossion ambaye ni Mbunge mteule wa ODM,na ambaye alisajiliwa kama afisa wa Knut na Msajili wa Vyama mwezi uliopita, anapinga uhalali wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Kitaifa ya (KnC) ambapo aliondolewa madarakani.

Kupitia wakili wake Judith Guserwa, Sossion aliiambia mahakama kwamba NEC ya Knut iliunda mkutano huo kinyume na sheria, na kunuia kumwondoa licha ya amri ya mahakama ya kusitishwa kwa mkutano huo na kuondolewa kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *