Hati ya Umiliki wa Tob Cohen Kusomwa Kesho

Tob Cohen lifts the Bronze Trophy Africa’s Best Golf Tour Operator 2018 at the 5th Wold Golf Awards Ceremony at La Manga Spain on November 3, 2018

Hati ya Umiliki wa hayati mholanzi Tob Cohen itasomwa kesho.

Barua kutoka kwa kampuni ya uwakili ya Kirundi & Company inasema kwamba Matakwa ya marehemu yatasomwa Ijumaa katika ofisi zao saa 11:30 asubuhi.Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya mwili wa Cohen kutambuliwa katika Hospitali ya Chiromo kufuatia uchunguzi wa Maiti.

Cohen atazikwa Jumatatu katika ibada ya kibinafsi kwenye kaburi la Wayahudi jijini Nairobi.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai wameulizwa  kuwezesha mpangilio uliowekwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *