Huduma za Kaunti Kurejea baada ya Rais Kutia sahihi Muswada wa Mapato

Rais Uhuru Kenyatta leo alitia saini na kuifanya sheria Sehemu ya Muswada wa Mapato 2019 na kuwezeshakuachiliwa kwa fedha kwa kaunti.

Sheria hiyo mpya imetenga Sh378.1 bilioni kwa serikali za kaunti kwa mwaka wa fedha wa 2019/20. Kati ya mgao wa jumla, Sh316.5 bilioni ni sehemu waliotengewa kutoka kwa mapato ya kitaifa wakati bilioni 61.6 ni mgao wa masharti kwa vitengo viligatuliwa.

Jumla ya Sh378.1 bilioni kwa serikali za kaunti ni asilimia 36.46 ya mapato yaliyokaguliwa na kupitishwa ya Serikali ya Kitaifa kwa mwaka wa fedha 2018/19 dhidi ya kizingiti cha katiba cha asilimia 15.

Hazina ya Kitaifa tayari imeshatoa zaidi ya Sh50 bilioni kwa kaunti ya miezi ya Julai na Agosti.

Baada na sheria hiyo mpya kuwekwa, Rais alisisitiza ahadi ya serikali yake kupeleka pesa katika kaunti kuwawezesha kuendelea kutoa huduma kwa Wakenya.
Alizitaka serikali za kaunti kukamilisha michakato yao ya bajeti ambayo inapaswa kuipa kipaumbele ugavi ya malipo kama vile KEMSA ili kuwezesha uhudumu wa huguma za afya .

Rais Kenyatta alizitaka serikali za kaunti kuunda mifumo bora ya kukusanya na kugawa mapato yao.

walioshuhudia kutiwa saini kwa Muswada huo walikuwa Kaimu mwenyekitiwa Uwekaji Hazina CS Ukur Yattani , waziri Eugene Wamalwa, Spika wa Bunge la kitaifa Justin Muturi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Kihara Kariuki na PS Dkt Julius Muia miongoni mwa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *