Shahidi Aliyejiondoa kwa Kesi dhidi Ya Dennis Itumbi Ashtakiwa

Shahidi aliyewasilisha ombi la kujiondoa kwenye kesi dhidi ya Dennis Itumbi alishtakiwa Alhamisi katika mahakama za Milimani  kwa kutumia hati zisizo halali.

Samuel Gateri alijiwasilisha mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Francis Andayi leo na kukanusha mashtaka mawili ya kutoa taarifa za uwongo na kutengeneza hati kwa nia ya udanganyifu.

Korti iliarifiwa kwamba mnamo Juni 20, 2019, Gateri alichapisha barua iliyosoma tarehe 30 Mei, 2019, na kunuia kuitumia kama hati halali iliyoandikwa na mmoja wa mawaziri. Gateri pia alishtakiwa kwa kuchapisha barua hiyo hiyo kwa tarehe zizo hizo.

Hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana ya pesa ya shilingi 100,000

Upande wa mashtaka ulisema kwamba jambo hilo litaunganishwa na lile la Dennis Itumbi. Jina la Gateri lilikuwa kati ya wale waliotajwa na kiongozi wa mashtaka kwenye kesi dhidi ya Itumbi.

Katika ombi alilowasilisha mapema mwezi huu, Gateri alidai kwamba alikamatwa mnamo Julai 2 na maafisa wa DCI ambao walichukua simu za rununu, kadi ya kitambulisho cha kitaifa, na vitu vingine vya kibinafsi.

Alidai maafisa hao walitishia kumpeleka kwa bwenyenye mkubwa zaidi katika vyombo usalama ili aweze kushughulikiwa.

Gateri alikamatwa katika hoteli moja jijini Nairobi ambapo alikuwa kwenye mkutano na wakili wake Georgiadis Majimbo na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Shauri Moyo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter wiki iliyopita, DCI ilisema Gateri alikuwa chini ya upelelezi na hakuwai orodheshwa kama wa shahidi wa serikali.

Walakini, jina la Gateri lilikuwa kati ya wale waliotajwa na kiongozi wa mashtaka katika hati ya mashtaka dhidi ya Itumbi. Gateri hapo awali alikuwa ameiambia korti kuwa maafisa wa polisi walimlazimisha akukubali kuwa alikuwa ameongea na Naibu Rais William Ruto katika kesi dhidi Itumbi kuhusu njama ya Hoteli La Mada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *