Naibu Gavana wa Kiambu Ashtakiwa Baada Ya kuwahamisha Wanakamati wa Kaunti

Kiambu Deputy Governor Nyoro sued for reshuffling Waititu's CECs

Mkazi wa Kiambu amewasilisha kesi kortini kupinga hatua ya Naibu Gavana wa Kiambu James Nyoro. Anamshtaki Nyoro kwa kuwahamisha Wajumbe wa Kamati ya Utendaji (CECs) kufuatia kusimamishwa kazi kwa Gavana Ferdinand Waititu.

Bernard Chege Mburu anasema kuwa gavana msaidizi anatumia madaraka ambayo hayamo kisheria, katika hatua hiyo anahofia kutokea kwa machafuko katika kaunti ya Kiambu kwani uhamishaji wa baraza la mawaziri haujaidhinishwa na kupitishwa kwani Gavana Waititu anaweza kuitupilia mbali atakapo rudi.

“Vitendo haramu vya Naibu Gavana vitasababisha hali ambayo itaathiri utoaji wa huduma kwa watu wa Kiambu kwani moja ya idara zilizoathiriwa ni Fedha,” inasoma hati ya korti.

Mpiga kura huyo anadai kwamba uamuzi wa Nyoro kufanya uhamishaji unaweza kuweka mfano hasi kwani huenda ukaigwa na naibu wasaidizi wengine iwapo wakubwa wao watalazwa hospitalini au kuenda likizo.

Katika usemi wake anohofia manaibu gavana wanaweza kuchukua nafasi ya magavana au kurekebisha Serikali ya Kaunti na mara baadaye kutupiliwa mbali na gavana  atakapo rudi.

Mburu anasema kuwa mnamo Septemba 6, 2019, Naibu Gavana wa Kaunti ya Kiambu alichapisha tangazo lililoashiria kuhamishwa kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaosimamia idara za malipo ya Fedha na Mipango ya Uchumi na Biashara, Utalii, Ushirika. na Maendeleo ya Biashara.

Mjumbe mtendaji wa Fedha na Mipango ya Uchumi Francis Kigo Njenga alihamishiwa hadi Idara ya Biashara, Utalii, Ushirika na Maendeleo ya Biashara.

Bwana Mburu Kang’ethe, ambaye alikuwa msimamizi wa Idara ya Biashara alipelekwa hadi Fedha na Mipango ya Uchumi .

Mkazi huyo anadai kwamba Nyoro, hana mamlaka ya kuteua, kumfukuza au kumhamisha afisa yeyote aliyeteuliwa na Gavana na kuidhinishwa na Bunge la Kaunti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *