Mamake mtoto wa Ken Okoth aashiria Kupinga Ubunge wa Kakake Marehemu

Mamake mtoto wa marehemu Ken Okoth, mjumbe mteuliwa Ann Thumbi, haonani na familia ya mbunge wa marehemu.Hii ni kutokana na hatua alichukua mnamo Jumanne.

Wiki chache baada ya Bernard Okoth kaka wa marehemu, kushikilia tikiti ya Chama cha ODM katika uchaguzi wa mchujo, Thumbi ameweka wazi anapendelea mpinzani wa mkwe wake kushinda katika uchaguzi.

Picha zinazozunguka kwenye mitandao ya jamii zimeweka wazi mapendeleo ya MCA huyo mteuliwa.

Thumbi anaonekana akiwa amevalia mavazi ya Chama cha Jubilee akiwa amejumuika na mgombea wa chama hicho McDonald Mariga. Picha hizi zilichukuliwa wakti mgombea huyo alipokuwa akiwasilisha idhini ya chama kwa IEBC.

Kitendo hicho kimewashangaza watumizi wa mtandao wa Kijamii,  wengi wakishangazwa na tendo lake la kukaidi mkwe wake.

Wengi wameonekana wakikemea kitendo hicho kwa vile alikuwa akienda kinyume na matakwa ya kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga.

Walakini, inasalia sinema upande ambao Thumbi atakaoegemea baada ya Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutupilia mbali idhini ya Mariga kuwania kiti hicho.

Ni muhimu kutambua, uamuzi wa Thumbi huenda ukawa umechochewa na mzozo unaoendelea kati yake na familia ya marehemu Okoth, baada ya MCA huyo kuenda kortini na kumtaka mwanawe kuorodheshwa kama mmoja wa wanaostahili kumridhi marehemu.

Kabla ya mazishi, Thumbi alikuwa ameanzisha mzozo mkali akitaka mwanawe kutambulika na kuhusishwa katika mipango ya mazishi ya Okoth.

Alienda kortini na kusaka amri ya korti kusitisha mazishi. Hata hivyo, siku moja baadaye Katibu Mkuu wa Chama cha ODM Edwin Sifuna, alitoa tamko kuwa walikuwa wamekubaliana kujadiliana nje ya vyumba vya Korti.

Hata hivyo, baada ya marehemu kuchomwa moto, Thumbi alisema hakuna makubaliano yoyote waliyokuwa wameafikiana.

Alirudi kortini na uchunguzi wa viinitete ulifanyika ambapo iliibuka kuwa mtoto alikuwa mwana halisi wa hayati mbunge huyo .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *