Watu maarufu Kenya ambao wamekuwa kwenye ajali kwa madai ya ulevi

Image result for de Matthew burial

Pombe imekuwa moja ya vinywaji vya kujiburudisha nchini na duniani kote imejulikana kwa kupunguza mawazo.

Licha ya hayo, pombe imechangia kwenye vifo vya mastaa na pia ajali zote humu nchini.

Mwanaharakati wa kibinadamu Boniface Mwangi aliamua kuanika watu ambao wamejipata kwa ajali barabarani juu ya kulewa chakari.

Wakenya wanajifanya sana. Tumefundishwa uoga na ukimya kama lugha. Wakati mtu anafanya vibaya, tunaangalia kwa njia nyingine na kujifanya hatuoni. Moja ya visanga vyetu kubwa ni ulevi. Tunayo watu wa familia ya walevi, marafiki, lakini hatuwahi kugombana nao au kuongea juu ya shida yao.

Hata Hivyo, Opera News iliamua kuweka orodha ya wasanii ambao wamewahi kupata ajali barabarani juu ya ulevi.

John DeMathew

Image result for de mathew burial

Mwanamuziki wa Benga John Ng’anga  almaarufu John DeMathew, aliangamia katika ajali ya barabarani mnamo Agosti 18, 2019 huko Blue Post.

Kulingana na Mwangi, DeMathew asingekuwa kwenye usukani akiwa mlevi asingekuwa maiti sas hivi.

Hakuna chombo cha habari au mtu yeyote serikalini, aliyetaja hiyo wakati walienda kwa mazishi yake. Boniface alizungumza na maafisa wa polisi ambao walikuwa wa kwanza kufika kwa ajali hiyo.

 

Joan Munyi (Yummy Mummy)

Akiongea kwenye mtandao wa Twitter mnamo Januari 2019, Joan alisema kwamba alikunywa kileo kadhaa cha whisky kabla ya kuchukua usukani. Alikubali kuwa ata hivyo hakuwa na ufahamu aliposhika usukani.

Rapa Wangechi

Image result for wangechi rapper

 

Kwa mwaka wa 2014, baada ya kupata chajio kwa sherehe ya rafiki wake na pia kunusurika kifo, Rapa Wangechi anasemekana alikuwa akiendesha gari akiwa mlevi. Alipoulizwa kuhusu hafla hiyo iliyosababisha kifo cha rafiki yake, Wangechi alisikitika kumpoteza rafiki wake.

Kwa kweli, sikumbuki mengi. Ninachokumbuka ni kula chakula cha jioni kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yangu na jambo lililofuata nilikuwa naamka hospitalini kama vile nilikuwa nimelala.

Image result for wangechi rapper

Mchungaji Ng’ang’a

Image result for accident pastor ng'ang'a

Mchungaji James Maina Ng’ang wa kanisa la Neno alikuwapo Jumatatu hapo hapo  ajali ya barabarani iliyohusika na gari yake na gari ya kibinafsi ambayo mwanamke (Mercy Njeri) aliuawa. Mchungaji Nganga, akaruka kutoka kwenye gari, akaifunga na kuingia ndani ya gari lingine ambalo lilikuwa nyuma na likatoka kwa kasi.

Image result for accident pastor ng'ang'a

 

Inspekta Mwala

Related image

Muigizaji wa televisheni na mtangazaji wa redio Davies Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala ndiye wa hivi karibuni kwenye orodha hii.

Inaripotiwa kwamba Mwala aligonga na kumuua mtu huko Kaloleni, kaunti ya Kilifi Jumatatu, Agosti 26. Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kilifi, Patrick Okeri, Mwala aligonga mtu huyo wa miaka 35 aliyetambuliwa kama Samwel Mwaki, na kumuua papo hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *