Wakenya wawili ni Baadhi ya Waathiriwa wa Machafuko Afrika Kusini- Monica Juma

A photo showing shops being looted

Wakenya wawili ni baadhi ya watu walioadhiriwa na vurugu dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Waziri wa Mambo ya Nje Monica Juma Jumatano alisema wawili hao ni kati ya watu kadhaa ambao mali yao imeharibiwa.

“Tuliamka na habari za kusikitisha kuhusu mashambulio ya chuki dhidi raia wa kigeni katika maeneo kadhaa nchini Afrika Kusini. Ripoti mikononi zinaonyesha Wakenya wawili waliathirika na mali yao kuharibiwa, “aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Alisema, Kenya inalaani vikali kuongezeka kwa wimbi wa mashambulio ya aina hiyo .Juma pia alisema ana matumaini kwamba maadili na uhasili wa kiafrika yatashinda yale kitaifa , na kuwa zitakuwa udi unaounganisha watu pamoja, kama ndugu na dada wa Kiafrika.

Alisema Ubalozi wa Kenya nchini Afrika Kusini unashauriana na Serikali kuhakikisha usalama wa Wakenya na ulinzi wa mali zao.

Juma alichapisha maoni hayo kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya kuwapokea na kufanya mkutano na Mhe. Jiechi Yang, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya COC na Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume kuu ya Mambo ya nje na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa China, katika afisi rasmi ya Wizara ya Mambo ya nje.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mnamo Jumanne alilaani wimbi la uporaji na ghasia ambazo zimelenga zaidi raia wa kigeni.

“Hakuwezi kuwa na sababu yoyote kwa raia wa Afrika Kusini kushambulia watu kutoka nchi zingine,” alisema.

Jumuiya ya Afrika (AU)pia ilitoa taarifa ikilaani “vitendo vya kuchukiza” vya dhuluma “kwa msimamo dhabiti”.

Jumatatu, Polisi walirusha vitoa machozi, risasi za mpira na mabomu ya kutetemeka katika juhudi za kumaliza machafuko . Kuongezeka kwa vurugu pia kumeshuhudia umati wa watu kulenga malori ambayo  yanaendeshwa na raia wa kigeni.

Vurugu ziliendelea Jumanne katika mji wa Johannesburg, kata ya Alexandra.

Hapo awali Balozi wa Kenya nchini Afrika Kusini Jean Kamau alisema raia kadhaa wa Kenya waliathirika na vurugu za hivi karibuni kupitia kuchomwa kwa mali yao na kupigwa.

“Tumewahimiza kufuata maagizo na kuitika wito wa polisi wa Afrika Kusini wa kuripoti matukio yoyote.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *