Mnong’ono Katika Chuo Kikuu cha Mara Baada ya Ufunuo wa Utapeli

Disquiet at Maasai Mara University following corruption exposé

Mnongo’ono unaendelea kushuhudiwa katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara katika Kaunti ya Narok kufuatia kufichuliwa kwa  uporaji wa pesa za umma kwenye taasisi hiyo. Uvumbuzi huo ulipeperushwa mnamo jumapili katika runinga ya Citizen TV.

Uchunguzi huo maalum uliyopewa jina la “The Mara Heist” ambao ulipeperusha mwendo wa saa  moja na saa tatu jioni. Uchunguzi huo uliangazia usimamizi wa chuo kikuu na tuhuma za utapeli wa Sh190 milioni kwa muda.

Uchunguzi zaidi wa Gazeti la The Standard uneonyesha kwamba watu wamekuwa wakinong’ona kichinichini katika makundi baada ya uchunguzi huo kuonyeshwa katika televisheni. Walakini, shughuli katika chuo hicho zimekuwa kama kawaida.

“Yote yako sawa. Tuko ofisini kama kawaida. Uvumbuzi huo haitatuzuia kutekeleza majukumu yetu,” mhadhiri mmoja alisema.
Alisema huenda kuna uezekano kukawa na nia fiche ya hadithi hiyo na inapaswa kuchunguzwa.

Aliyeangazia utapeli huo, kaimu Meneja wa Fedha wa chuo kikuu Spencer Sankale, alivumbua jinsi dereva wa Chancellor Prof Mary Walingo, Hassan Noor alivyotumiwa kama chombo katika wizi huo.

Afisa Maswala wa Kampuni ya Chuo Kikuu hicho Amosi Kemboi aliliambia gazeti la The Standard kuwa yote alikuwa shwari licha ya Ufunuo huo.
“Kila kitu kiko sawa hapa. Chuo kikuu ki salama na shughuli za kuwaandikisha wanafunzi wa mwaka kwanza zinaendelea ,” alisema Bw. Kemboi.

Aliongeza pia kuwa chuo hicho kiko tayari kuandaa  Mkutano wa siku mbili wa Sayansi na Utafiti. Hata hivyo,Wakenya katika Mtandao wameendelea kukejili wahusika  wakiimtambua mkuu wa chuo hicho kama ‘ng’ombe mkubwa’ anayehitaji nyasi, wakati nyasi inamaanisha pesa kama ilivyonukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *