Fahamu mengi kuhusu mchungaji billionea Ng’ang’a

Image result for PASTor nganga

Wakenya wengi wanamjua mchungaji Ng’ang’a wa kanisa la Neno jijini Nairobi kwa namna amekuwa akiendesha shughuli zake za ukristo kwa njia inayoshangaza.

Sio kwa mara moja au mbili bali mara nyingi amegonga vichwa vya habari kwa makosa au mazingaombwe yanayoendelea kanisani mwake.

Hata hivyo, Ng’ang’a alielezea hivi karibuni kuwa waumini wa kanisa lake hawawezi wakamwacha kwani wanampenda na kumheshimu.

Opera News ilifanya uchambuzi wa kina na haya ni baadhi ya mambo ambyao hukuwa unayafahamu kumhusu mchungaji Ng’ang’a.

Image result for PASTor nganga

Kwa mujibu wa Daily Nation, Ng’ang’a alikaa zaidi ya miongo miwili gerezani, kwa kuwa mhalifu mkali. Ripoti kutoka rekodi mbalimbali, hata hivyo, zinatofautiana kwa vipindi ambavyo alihukumiwa.

Ng’ang’a alizaliwa Subukia, Kaunti ya Nakuru, mnamo 1954, alihukumiwa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 18 mnamo 1972.

Kulingana na mchungaji kupitia mahojiano ya Radio Jambo Agosti 13, alihukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kupigana.

Nakala iliyotangazwa na kituo chake cha Sasa TV, ilisema kwamba aliwekwa kizuizini mnamo 1968 akiwa na umri wa miaka 14.

Ng’ang’a aliona mwanga na kumpokea Yesu gerezani, tukio ambalo alitaja kama siku alipiga hatua. Kisha akaanza kusukuma mikokoteni na kuhubiri katika mitaa ya Mombasa. Wakati wafuasi wake walipokua, alihamia Nairobi ambapo alianzisha kanisa lake la NENO.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *