Inspekta Mwala aomba msamaha shingo upande kwa familia ya jamaa ailyemuua

Image result for inspekta mwala

Muigizaji wa sinema Davies Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala mwishowe ameomba msamaha kwa familia ya mtu aliyemuua katika kaunti ya Kilifi.

Kama tulivyoripoti hapo awali, Mwala aligonga na kumuua mtu wa umri wa miaka 35 kwenye kaunti ya Kilifi.

Kwenye chapisho la Twitter, muigizaji wa Citizen TV alisema hakukusudia kumuua mtu huyo na kama angekuwa muuaji, angejiunga na wanamgambo wa Al Shabaab.

Image result for inspekta mwala

“Samahani kwa kile kilichotokea na poleĀ  kwa familia, ikiwa mimi ni muuaji, basi ningekuwa nimejiunga na al-Shabaab, hatua yangu ni ..tukuwe watu wenye msingi, watu wetu wengine wanakufa kwa njaa na haujawahi kuongea juu ya hayo kwa njia ambayo umefanya, “alisema

Kamanda wa polisi wa Kilifi, Patrick Okeri alisema muigizaji huyo wa radio ya Citizen alikuwa akiendesha kutoka mji wa Kaloleni kwenye Barabara kuu ya Mazera wakati ajali hiyo ilitokea.

https://twitter.com/inspektamwala/status/1167303327203254272?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1167303327203254272&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.tuko.co.ke%2F314166-inspekta-mwala-apologises-family-pedestrian-killed-accident.html

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *