Wakenya wamkejeli Waziri baada ya Kusherehekea Msaada kutoka Uchina

Image result for CS Wamalwa

Waziri wa Ugatuzi, Eugene Wamalwa Jumatano jioni, aliipandisha mizuka ya Wakenya alipodhibitisha katika ukurasa wake wa Twitter kwamba Kenya ilikuwa imepokea mifuko 30,000 ya mchele kutoka Uchina. Mifuko hiyo ya mchele inanuiwa kusambazwa kama chakula cha msaada katika kaunti 23 zinazoathiriwa na ukame.

“Nimepokea msaada wa mifuko 30,000 ya mchele kutoka Jamhuri ya Watu wa Uchina itakayo ongezwa kwa chakula cha msaada wa Serikali katika kaunti 23 zilizoathiriwa na ukame.” Usemi ulisoma.

Ishara hii ya ukarimu ya WaChina, hata hivyo, haikuwapendeza Wakenya wengi waliomkejeli na kuelezea kwamba China imekuwa sura mpya ya ukoloni mamboleo nchini Kenya na waliikemea serikali kwa kupokea msaada kutoka kule.

Mtumiaji wa Twitter anayejiita Mkaazi Langata alisema, “Eugene Wamalwa unaonekana kufurahi sana hadi unaweka chapisho hili?Je,ni miaka ngapi baada ya uhuru?”

Hizi hapa baadhi ya mawazo ya wakenya waliojawa na kejeli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *