Ezekiel Mutua apiga marufuku Wamlambez na Tetema

Image result for ezekiel mutua

Polisi wa maadili, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya (KFCB), Ezekiel Mutua ametoa agizo juu ya kuzuia kuchezwa kwa mziki wa  Wamlambez na Tetema.

Kupitia taarifa kwenye Twitter, Mutua alisema kwamba ni marufuku kucheza Wamlambez na Tetema nje ya vilabu na baa.

Aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata viongozi wakiimba na kucheza huu mziki jukwaani na kwenye hafla zao.

Viongozi hao ni pamoja na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, mwakilishi wa zamani wa wanawake wa Nairobi Rachel Shebesh, mke wa kwanza wa Machakos Lilian Ng’anga, miongoni mwa wengine.

Wimbo wa Tetema uliachiliwa mnamo Februari mwaka huu na umekuwa kwenye orodha za kucheza na MaDJ wengi wa Kenya kutokana na mdundo wake wa kutamanisha.

Image result for tetema

“Inatia aibu kuona hata viongozi wa kitaifa wakiimba na kucheza kwa midundo hiyo hadharani. Nyimbo ni chafu na haifai kwa matumizi ya umma, haswa watoto,” alisema Mutua.

Wamlambez ya kikundi cha Sailors imekuwa maarufu sehemu nyingi duniani na kwa njia fulani imekuwa alama kwa Wakenya wengi nje ya nchi.

Hii pia inafuata tukio la mnamo Aprili mwaka huu, ambapo Mutua alipiga marufuku wimbo wa Takataka baada ya vifo vingi vya wanawake kushuhudiwa na kile ambacho kilidhamiriwa kuendelezwa juu ya matamshi ya wimbo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *