Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, Jumapili usiku, alichemka baada ya mtangazaji wa K24 TV, Anne Kiguta kumuuliza maswali za kibinafsi wakati wa mahojiano.
Mtangazaji huyo shupavu alirejelea suala la Sonko la hivi karibuni ambapo alijibizana kwa maneno makali na Mwakilishi wake wa wanawake, Esther Passaris, na mbunge wa Suba Kaskazini, Millie Odhiambo.
Kiguta alisisitiza tukio ambalo Sonko alimshambulia Passaris mbele ya umati wa watu akidai kuwa hakuwa na mwelekeo wa kupokea simu zake kwa kuwa yeye sio mume wake.
Hapo awali alikuwa amechapisha kwenye mtandao wa Facebook akilaani afya ya uzazi ya Millie baada ya kumshtumu kwa kuanzisha shambulio dhidi yake.
Kama kwamba hajafurahishwa na maoni yake, gavana alimkumbusha mtangazaji kuwa alikuwa anaenda mbali sana na kwamba alikuwa akiuliza maswali yasiyofaa.
Alifikia wakati ambapo alimwambia Kiguta kwamba yeye sio mume wake kama tu alivyofanya kwa Passaris.
.@MikeSonko: …even wewe, mimi si bwana yako, that is a reality, sio matusi!#SonkoOnPunchline #Punchline w/ @AnneKiguta pic.twitter.com/kojS0Bz3Db
— K24 TV (@K24Tv) August 25, 2019
.@MikeSonko: Millie said…#SonkoOnPunchline#Punchline w/ @AnneKiguta pic.twitter.com/r9EGFcaguM
— K24 TV (@K24Tv) August 25, 2019