Madaktari Wamtoa Buibui Mwenye sumu Kutoka kwa Sikio la Mwanamke

Image result for a brown recluse spider

Mwanamke mmoja kutoka Missouri Marekani aliponea chupu chupu  baada ya buibui mwenye sumu kutambaa ndani ya sikio lake wakati alikuwa amelala. Susie Torres anaishi Kansas City aligundua yote si shwari alipoanza kuhisi  maumivu Jumanne asubuhi katika sikio lake.

“Niliamka Jumanne nikisiskia kana kwamba kuna maji kwenye sikio langu la kushoto. ina ufananisho kana kwamba unapotoka kuogelea na unayo maji kwenye sikio lako, ” Torres akiambia kituo cha  runinga cha WDAF-TV nchini humo.

Torres alipokwenda kwa daktari wake ili kujua ni nini baya, Daktari msaidizi katika hospitali hiyo alipigwa na butwaa na kushindwa cha kumweleza Susie.

“Alikimbia na kusema anawaendea watu wengine zaidi. Kisha akasema, ‘Nadhani unayo wadudu kule,’ “alikiambia kituo cha KSHB-TV.

Kilichotokea baada daktari kurudi chumabani kilimshtua Torres.

Image result for Susie TorresSussie Torres alipatikana na buibui kwenye sikio lake la kishoto

 

“Alirudi ndani na kuniambia nilikuwa na buibui aliyekuwa akitengeneza utando wake kwenye siko langu ,” Torres alisema huku akikiri kuwaogopa viumbe wale.

Madaktari walifanya ukarabati wao na kumtoa kiumbe yule mwenye mate ya sumu. Kulingana na Vituo vya Udhibiti wa Magonjwa, buibui yule akakuuma anaweza kusababisha maumivu na vidonda vikali ambavyo vinahitaji  matibabu ya upesi.

Kwa bahati nzuri, buibui yule hakumuuma Torres.

Kutoka na kisa kile Susie Torres ameapa kuchukua hatua ya kujikinga na kisa kama hicho

“Nilikwenda na kutia mipira ya pamba masikioni mwangu jana usiku. Ninavua nguo zangu zote na kuzitikisa kabla ya kuzivaa. Mkoba wangu pia nimeacha kuuweka sakafuni. Nimekuwa  mwangalifu zaidi, ” aliiambia runinga ya WDAF-TV.

Imesalia fumbo,jinsi na lini bubui yule allinigia kwenye sikio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *