Mamia wakusanyika huko Gatanga kwa mazishi ya John De’Mathew

John DeMathew

Waombolezaji walikusanyika huko Gatanga, Kaunti ya Murang Jumamosi kumuaga kwaheri mwanamuziki wa kisasa wa benga John Ng’angamba Mwangi almaarufu John De’tMathew.

Mazishi iliyofanyika katika Shule ya Msingi ya Githambia ilianza saa 10 asubuhi.

De’Mathew aliaga dunia katika ajali ya barabara karibu na Jiji la Thika Jumapili usiku.

Image result for de mathew
Picha: Kwa Hisani

Tangu habari ya kifo chake kutangazwa, risala za zambirambi zimekuwa zikiongezeka kutoka kwa wanamuziki wenzake, mashabiki na viongozi wa kisiasa kutoka nchi nzima.

DeMathew, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tamco Sacco iliyozinduliwa hivi karibuni, alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwa mkutano wa kufadhili pesa kwenye bar ya Metro Fill jijini wakati alipokutana na mauti.

DeMathew atakumbukwa sana kwa mziki wake maarufu inayoitwa Peris Nduku iliyovuma mwaka wa 1987 na hadi kifo chake mziki wake umetambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *