Orengo akimbia Mahakamani Kuzuia Kukamatwa kwa Tabitha Karanja

Image result for james orengo in court

Mkurugenzi Mtendaji wa Keroche Breweries, Tabitha Karanja, na mumewe, Joseph Karanja, sasa wameenda kortini wakitaka kusimamisha kukamatwa kwao kwa madai ya ulaghai wa kodi ya shilingi 14 bilioni.

Kupitia wakili wao, Seneta James Orengo, wanataka mahakama kuu imzuie DPP Noordin Haji kutowashtaki kwa makosa kumi ambapo anayeshtaki anasemekana alipoteza mapato ya kodi.

Habari inayofikia Opera News ni kwamba wafanyibiashara hao walitumia usiku huo katika ofisi zao huko Naivasha kwani maafisa wa DCI na KRA walipiga kambi katika jumba hilo.

Image result for tabitha karanja

Siku ya Jumatano jioni Tabitha alisema kwamba hatajiwasilisha kwa maafisa baada ya hati ya kukamatwa ilipotolewa dhidi yake, kwa madai ya kukwepa ushuru wa bilioni 14.

Mjasiriamali huyo pia alilia kwa serikali juu ya madai ambayo yeye huyaita kama hayana msingi na maana ya kumdhalilisha.

Unaweza kufikiria, nimefuata sheria, nimefanya kazi miaka hii yote na halafu unapata WhatsApp, hata hakuna mawasiliano rasmi, ya kuambiwa kwamba una deni la serikali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *