DPP aamuru wakurugenzi wa Keroche, Tabitha Karanja na Mumewe kufikishwa mahakamani… Pata Maelezo kwa kina

Tabitha Karanja

DPP ameamuru  wakurugenzi wa Keroche Breweries Ltd Kufunguliwa mashtaka ya ukwepaji wa kodi ya Shilingi 14.45  bilioni. Wakurugenzi ni Tabitha Mukami Mungai na bana yake Joseph Karanja.

Katika taarifa yake Jumatano, DPP Noordin Haji alisema uchunguzi umebaini wawili hao amejihusisha na makosa 10 ya udanganyifu wa kodi.

Noordin Haji ilisema kuwa kamishna Mkuu wa KRA aliwasilisha faili ya uchunguzi ofisini mwake mnamo Agosti 18 na ukaguzi uliofanywa na KRA ulidhihirisha kwamba Kampuni ya Keroche Breweries imekwepa malipo ya ushuru ya jumla ya sh14,451,836,375.

Kampuni hiyo inatuhumiwa kutolipa malipo ya mihuri VAT ya Sh12.34 bilioni , (Sh329.4 milioni), Crescent Vodka (Sh135.4 milioni) pamoja na bidhaa zingine. Keroche pia anatuhumiwa kukwepa malipo ya ushuru wa forodha wa jumla ya Shilingi bilioni 2 kwa vitu hivyo hivyo.

DPP alisema ameridhika kwamba kuna ushahidi wa kutosha kushtaki watuhumiwa hao kwa makosa 10 ya udanganyifu wa kodi kinyume na Sheria ya Taratibu za Kodi ya 2015.

Kwa hayo aliamuru wakurugenzi kufikishwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *