Uchuguzi wa Daktari wadhihirisha sababu ya Kifo cha De’Mathew

John-DeMathew

Marehemu John Mwangi Ng’ang’a anayejulikana John De’Mathew alikufa baada ya mbavu zake kuvunjika na ini yake na kongosho kuharibiwa, ripoti ya Daktari imedhihirisha.

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Bwana Muherali Kariuki, alisema ukaguzi wa maiti uliofanywa siku ya Jumanne, umedhihirisha kwamba mbavu za marehemu zilivunjika vibaya baada ya ajali mbaya baada ya gari lake kugonga lori huko Blue Post huko Thika.

“Ripoti ya Uchuguzi ya maiti  imeonyesha kuwa viungo vya ndani – ambavyo ni mapafu na kongosho – viliharibiwa vibaya baada ya mbavu zote nane kuvunjika na kuathiri viungo vya ndani,” Bwana Muheria alisema.

“Kutokana na matokeo ya uchunguzi wangu, ni maoni yangu kuwa sababu ya kifo ni majeraha ya tumbo kutokana na nguvu ya kiwewe inayoandamana na ajali za barabarani,” ripoti iliyosainiwa na mtaalam waupasuaji wa maiti, Dorothy Njeru

Muheria pia alitangaza kwamba maandalizi ya mazishi ya  marehemu yameanza na mikutano inafanyika huko Blue Springs, Metro Club Thika.

Waombolezaji pia wanakutana katika nyumba mbili za mwanamuziki huyo. Kundi moja lina kutana katika Makao ya Githingiri, ambapo mkewe wa kwanza Sarafina Mwangi anaishi, na nyumbani kwa Mukurwe ambako mkewe wa pili, Caroline Waithira.

Bwana Muheria aliliambia Gazeti la Nation kuwa marehemu atazikwa Jumamosi katika kijiji cha Mukurwe na viongozi wa kitaifa, pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, anayetarajiwa kuhudhuria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *