Ng’amua ukweli kumhusu John De Mathew

Image result for de mathew

Jioni ya Jumapili, Agosti 18, jamii ya Kikuyu na tasnia ya muziki wa mitaa kwa ujumla walipoteza msanii mwingine wa kihistoria.

John Ng’ang’a Mwangi almaarufu De Mathew aliaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabara kwenye Blue Post barabara kuu ya Thika.

Hata ingawa alikuwa maarufu kwenye eneo la mlima Kenya, baadhi ya watu hawamtambui De Mathew sana na haya ni baadha ya mambo kumhusu ambayo unafaa kuyang’amua.

Familia

John Ng’ang’a Mwangi alizaliwa katika kijiji cha Gathiru-ini, eneo ndogo la Mukurwe-ini katika jimbo la Gatanga, kaunti ya Murang’a karibu miaka 50 iliyopita.

Alikuwa mwana wa Mathayo na marehemu Wanjiku. Jina lake De’Mathew liliundwa kutoka kwa baba yake.

Alikuwa mzaliwa wa nne katika familia ya ndugu zake wanane.

Image result for de mathew

Wake na Watoto

De Mathew alioa wanawake wawili; Sarafina na Caroline Waithera na ameacha nyuma wana watatu.

Masomo

Mwanamuziki marehemu alianza masomo yake katika shule ya msingi ya Mukurwe-ini (hivi sasa Githambia).

Aliendelea na Sekondari ya Naaro huko Kandara na pia akasomea Shule ya Sekondari ya Igikiro.

Kazi ya mziki

Kulingana na wale waliomjua vyema na kwa kiwango cha kibinafsi, De’Mathew alitunga wimbo wake wa kwanza wakati bado alikuwa Darasa la Saba.

Kazi yake ya muziki ilianza rasmi mnamo Desemba 1986 kwa msaada wa Timona Mburu na Joseph Wamumbe na akaachilia wimbo wake wa kwanza.

Alianza kuachia wimbo wake wa My Dear Nduku mnamo Agosti 1987 ambao ulimtambulisha kwa mziki na kumpatia umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *