Washirika wa Raila, Ruto wapimana nguvu kwenye mazishi ya mwana wa mbunge

Siasa zilitawala wakati wa mazishi ya aliyekuwa afisa wa baharini Marekani Chris Masaka, ambaye ni mwana wa mbunge wa Ikolomani Bernard Shinali Ijumaa na wanasiasa wakiweka ajenda zao mbele ya 2022.

Pamoja na mbio hizo kufikia sasa, inaoneana wazi kuwa ni pande ya naibu rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga zina nia ya kugawanyika kabla ya uchaguzi mkuu.

Echesa, mshirika wa karibu wa Daktari Ruto, alimshutumu Bw Odinga kwa kutumia handisheki kunufaisha Nyanza  licha ya kupata msaada kutoka mkoa wa Magharibi.

Image result for william ruto on referendum

Lakini mbunge wa Budalang’i Raphael Wanjala wa ODM alimpinga Bw Echesa, akitaka kujua alisaidiaje mkoa wakati anahudumu kama katibu wa baraza la mawaziri.

Ruto, ambaye pia alikuwepo, alikuwa amewaambia viongozi wa kisiasa wasitumie mjadala wa kura ya maoni ili kuleta mgawanyiko kwa Wakenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *