Machafuko yatokea huku vijana wavuruga kituo cha sensa Kangemi

Image result for kangemi residents raid census center

Mvutano yakaza mwendo Kangemi katika Jimbo la Westlands baada ya wakaazi kuenda barabarani Alhamisi kuandamana wakilitia doa kuajiriwa kwa maafisa wa sensa katika eneo hilo.

Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya vijana waliofurika kituo cha mafunzo ya sensa katika shule ya msingi Kihumbuini huko Kangemi, kaunti ya Nairobi kukosoa harakati iliyotumiwa watu kupata kazi.

Kulingana na wakaazi, wengi wa waendesha shughuli ni kutoka Eastlands.

Image result for tim wanyonyi
Tim Wanyonyi

Mjumbe wa Bunge la Westlands Tim Wanyonyi hata hivyo alisema kuwa mchakato huo hautaendelea, hadi usajili utakapokaguliwa.

Hii inakuja wiki moja baada ya wakaazi watano wa Kaunti ya Homa Bay kufika kortini wakitaka kuisimamisha Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ya Kenya (KNBS) kutekeleza zoezi la sensa katika kaunti hiyo wakishinikiza kuwa watu ambao hawakuwa kwa orodha ya kuomba kazi ndio waliopata kazi.

Katika sensa ya mwaka huu, jumla ya wafanyikazi 174,700 wanatajiriwa kwa zoezi lililowekwa kufanywa Agosti 24 na 25, 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *