Umesaliti Mrengo wa NASA na wafuasi wako wote- Ndii kwa Raila

Image

Mbunifu wa Nasa, David Ndii, ametaja Raila Odinga kama msaliti kwa wafuasi wake wote baada ya mkutano wake na dada ya Rais Uhuru Kenyatta, Kristina Pratt Kenyatta.

David Ndii ameelezea kwamba mrengo mzima wa Nasa na wafuasi wake wamesikitika  kabisa.

Wawili hao walifanya mazungumzo katika ofisi za Raila Odinga kule Capitol Hill,  maelezo kuhusu mkutano huo wa kipekee yamesalia wali wa daku.

Kristina Pratt alikuwa mjumbe katika uchaguzi mkuu wa 2017 ambapo aliwasihi wakenya wampigie kura kaka yake Uhuru Kenyatta. Pratt na Muhoho Kenyatta wamekuwa nguvu ya Uhuru hadi sasa.

Kulingana na David Ndii, Raila amewasaliti Wakenya wengi ambao walijitolea sana kumpigania. Wengi wao wakiteswa na hata wengine kuuawa katika kupigania haki za uchaguzi nchini Kenya.

Mawazo haya ya David Ndii yameibua majibu mengi kutoka kwa watumizi wa mtandao wa twitter.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *