“Sitawai wania ubunge wa Kyandondo tena” – Bobi Wine

Image result for bobi wine

Mbunge wa Kyandondo Mashariki Robert Ssentamu almaarufu Bobi Wine ameapa ya kwamba hatawahi wania ubunge wa eneo hilo tena.

Akiongea Lusanja kwenye maadhimisho ya kila mwaka tangu dereva wake Yasin Kawuma kuaga dunia, alisisitiza kuwa kwa sasa hivi, ako na adui mmoja tu na azma yake ni kumwondoa Museveni.

Sitasimamia ubunge wa Kyandondo Mashariki tena, sasa hivi niko na misheni kubwa, na hiyo ni kumwondoa dikteta mkuu Museveni

Bobi Wine aliongeza kuwa siku ambayo Yasin Kawuma alipigwa risasi Arua, Agosti mwaka jana, inafaa kupelekea watu kusukuma ajenda ya kumwondoa Museveni.

Image result for bobi wine in court

Yasin Kawuma hakuwa mwanasiasa na aliuliwa. Mimi sio mtumwa wa serikali yoyote na situmikii watu kwenye serikali. Nina msimamo wangu kibinafsi. Tunafaa kujua kwamba sio kwa mujibu wa serikali bali sisi sote, tupiganie uhuru wetu.

Matamshi hayo yanakuja muda mfupi baada ya kutangaza azimio lake la urais wa mwaka wa 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *