“Mama yangu anateseka,” Wendy Waeni afichua meneja wake tapeli, Joe Mwangi

Wendy Waeni

Wendy Waeni ambaye ni mwanasarakasi tajika ameshtua taifa baada ya kufichua meneja wake wa zamani Joe Mwangi kama mtu tapeli.

Wendy aliibuka miaka michache iliyopita na amejulikana kwa kufanya sarakasi na kuigiza kwa wakuu wa nchi kadha wa kadha.

Hivi karibuni alipata nafasi akiwa na Joe Mwangi, kuigiza kwa rais Kenyatta, mwenzake Kagame, na hata akasafiri kwenda China na sehemu zingine za ulimwengu.

Image result for wendy waeni

Walakini, Wendy Waeni tunayemwona kwenye mitandao ya kijamii sio Wendy halisi, meneja wake wa zamani Joe Mwangi amekuwa akiposti picha zake Waeni na hata kutoa maoni yake kwenye mitando.

Mwaka wa 2017, kupitia ukurasa wa Waeni wa Instagram, video iliwekwa mwanaarakasi huyo akilindesha na kufurahia ‘Range Rover Velar mpya’ ambayo wafuasi wake walisifia kuwa kwa kweli, ‘Amefika’.

Wakenya kwenye Twitter walishtushwa na ufunuo wa Wendy ambao wameona kwamba Joe Mwangi amekuwa akimtumia vibaya ili kujinufaisha mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *