Jimmy Gait afichua kwa nini anaenda kufanyiwa upasuaji India

Image result for jimmy gait

Msanii wa injili Jimmy Gait amepanga kusafiri kwenda India kwa matibabu juu ya shida ya koo ambayo imekuwa ikimuathiri kwa mwaka sasa.

Jimmy ambaye anafahamika sana kwa wimbo wake wa ‘Muhadara’ alisema kuwa atakuwa India kwa siku 15-20 kwenye mahojiano na jarida humu nchini.

Nilienda hospitali mwaka jana kwa sababu singeimba ama ata kuongea kwa nguvu. Ninaenda kwa matibabu, nitakwenda India siku ya Jumapili. Nilikuwa nimelazwa kwenye hospitali ya Aga Khan kwa siku kadhaa daktrai akifanya ukaguzi ndo maana kumekuwa na picha zinasambaa mtandaoni.

Ameongeza kuwa haikuwa njia rahisi kwake kwani mziki ni kazi yake na anaipenda.

“Hii imeathiri kazi yangu ya mziki na ninatumai kuwa yote yatakuwa sawa ninapoenda India ili kurudi kwa mziki,” aliongezea.

Kulingana na msanii huyo wa injili, kuumwa kwa koo yake imemsababishia kutoimba kwa mwaka moja sasa maanake haitamruhusu.

Aliendelea kuwashauri wale wanaodai kuwa yeye ni mtu anayetafuta kiki kuelewa kwamba maswala mazito kama ya kiafya sio mambo ya kufanya mzaha.

“Nawasihi watu wanipe motisha ninapopitia changamoto haya. Sijawahi kuwa kwa upasuaji mbeleni kwanza inapokuwa kwa sehemu ya muhimu sana ya mwili wangu inanifanya niwe na wasi wasi”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *