Msaidizi wa Bobi Wine aaga, jicho lachomolewa

Image result for ziggy wine

Michael Kalinda almaarufu Ziggy Wine ameaga baada ya majeraha ya mateso na kuchomolewa jicho.

Ziggy Wine aliripotiwa kutekwa nyara mnamo Julai 21, 2019 na watu wasiojulikana mpaka aliopatikana ametupwa karibu na hospitali ya Mulago wiki baadaye lakini akiwa katika hali mbaya na jicho lake la kushoto lilichomolewa na vidole viwili kukatwa.

Alikimbzwa kwa Hospitali ya dharura ya Mulago ambapo alipokea matibabu hadi wakati alihamishiwa katika kituo cha afya cha kibinafsi na marafiki wa karibu na familia.

Image result for ziggy wine

Kulingana na ripoti kwa mmoja wa familia ambaye alipendelea kutokujulikana, mabadiliko hayo yalitokana na vitisho ambavyo walipata kutoka kwa watu wasiojulikana.

Polisi waligundua kuwa Ziggy Wine alikuwa na vidonda vya moto juu ya mwili wake wa juu ambao inasemekana kutoka kwa chuma.

Mnamo Jumamosi Agosti 3, Msemaji wa Metropolitan wa Kampala, Patrick Onyango alisema kuwa polisi walikuwa bado hawajapata ripoti zozote kuhusu utekaji nyara kwa sababu familia ilikuwa imechagua kunyamaza. Hata hivyo alibaini kuwa polisi walipaswa kuanzisha uchunguzi katika suala hilo ili kuwaleta watuhumiwa na haki ipewe Ziggy.

Ziggy Wine alikuwa msanii wa muziki na meneja wa vyombo vya habari katika kikundi cha burudani cha Fire Base Entertainment ambacho kinaongozwa na mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi almaarfu Bobi Wine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *