Acha muziki! Msanii Pitson ashauriwa na madaktari

Image result for pitson

Mwimbaji wa injili Pitson ameshauriwa kuacha kuimba kwa miezi michache ijayo baada ya sauti yake kuleta utata.

Kulingana na msaii huyo, madaktari walimshauri kuwa hapaswi kuimba kwa miezi chache zijazo.

Nilienda kwa daktari na waliniambia itabidi nichukue muda wa miezi miwili ili kumzisha koo yangu na sitaweza kuimba kwa muda huo

Image result for pitson

Madaktari walisema amekuwa akifanya kazi sana na koo lake limeleta utata, ambayo ilisababisha uharibifu.

Akiongea na Word Is siku ya Ijumaa, mwimbaji huyo alisema ni lazima anywe maji mengi na pia apumzike sana.

Mziki ni kitu ambacho nakifanya kama kazi na nakitegemea, kuacha itakwa balaa kwangu

Kabla ya kushauriwa asiimbe, Pitson alikuwa amerekodi wimbo ambao atakuwa akiutoa katikati ya Agosti.

Msanii wa Tanzania Ommi Dimpoz pia amewahi kuwa na shida hiyo na alienda Ujerumani kufanyiwa operesheni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *