Bahati ajibu madai ya kusainiwa na Wasafi (WCB)

Image result for Bahati in 707 gatsby

Msanii wa injili Kevin Bahati almaarufu mtoto wa mama ambaye pia ni bosi wa lebo ya Eastlands Most Beloved (EMB) amekanusha madai kuwa anataka kujiunga na Wasafi (WCB).

Msanii huyo akihojiwa kwenye kituo cha Milele alisema yeye ni msanii waziwazi wa injili alipoulizwa na Alex Mwakideu pamoja na Jalang’o kuhusu ziara zake za mara kwa mara kwa taifa ya Tanzania na familia ya Wasafi.

Bahati alijibu akisema kuwa anapenda kumtembelea Diamond Platinumz ili kujifunza mambo kuhusu biashara na jinsi ya kuendesha lebo vizuri maana mkuu wa Wasafi anashikilia lebo kubwa Afrika.

Image result for bahati and diamond platnumz

Aliongezea pia kuwa ana uhusiano wa kibiashara na Wasafi na baadhi ya mabadiliko ambayo amefanya kwa mziki wake umetokana na kujifunza kutokwa kwa Wasafi.

Mimi kuenda Wasafi kwa uhakika ni kwa sababu ya biashara na unajua bila shaka kuwa Wasafi ni moja kati ya lebo zilizofanikiwa barani Afrika na kuwa Rafiki wa mtu kama Diamond utajifunza mengi na nikitoka hapa kwenda Tanzania, naenda kutulia na kuskiza.

Image result for bahati and diamond platnumz

Bahati alisisitiza kuwa anajifunza kutoka kwa wasanii waliomtangulia na Diamond Platinumz ni mmoja wao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *