Slayqueens waduwaa baada ya Kamene Goro kupuuza milioni 100

Image result for kamene goro

Mwanahabari mashuhuri Kamene Goro amekiri kuwa amejua ni kwa nini vidosho hupata maisha ya raha mustarehe na kukaa kwenye makazi ya kifahari bila kuwa na kazi inayojulikana.

Hata hivyo, amesema kuwa hayuko tayari kufuata njia hiyo maanake hiyo sio mahali anataka kuelekea.

Hivi majuzi, Kamene alimsingizia Huddah Monroe kuwa anafanya kazi ‘chafu’ ili kupata pesa na pia kupata kuzunguka ulimwengu.

Image result for kamene goro

Akiweka haya wazi, Kamene aliweka picha akionyesha jinsi mwanaumme alimwomba kuwa na mapenzi na yeye ili alipwe dola miliona moja (milioni mia moja za Kenya = 100,000,000). Hii inajumuisha kufanya mapenzi nae na kufanya maziara za hapa na pale.

Picha ya maelezo ya matakwa ya mwanaume huyo Picha: Kwa Hisani

Kamene Goro alipuuza matakwa ya jamaa huyu akisema hawezi akataka maisha haya na akaomba apate pesa za kweli na haki.

“Kwa hivyo nadhani hii ni jinsi watu wengine wanavyofanya kazi na kunufaika… .Hii ilikuwa kwa DM yangu asubuhi ya leo… .. Milioni 100 ni Pesa nyingi, Mungu wangu, mzigo wa pesa, lakini MUNGU WANGU ANAFANYA KAZI ZAIDI, KUPATA $ 1MILIONI YANGU INAENDELEA KUTOKA KAZI YANGU. Wasichana, wacha niwaambie, kitu chochote mwanaume yeyote atakupa kwa kumpatia mwili wako, BWANA MUNGU atakupa zaidi ya mara kumi kutoka kwa kazi yako! Nakuahidi!! Kataa! kataa! kataa! Mungu anajitahidi sana kufanya ndoto zako zitimie, hauitaji kueneza miguu yako ili upate bakuli ya dhahabu mwishoni mwa mvua.

Uamuzi wa Kamene umezua gumzo mtandaoni na cha kushangaza ni kuwa wanawake wengi wameshawishi kukubali mwito huo.

Itakumbukwa kuwa Kamene Goro miaka miwili yaliyopita, alikiri kuwa amefanya mapenzi na zaidi ya wanaume 27 kabla ya mwaka huo.

Haya ni baadhi ya maoni ya wafuasi wake;

paul_mugz

Chukua hii pesa tupunguze deni ya Mchina😂😂

stacey_kigo

Kamene!Kamene!Kamene!nimekuita mara ngapi???take the money and run.such opportunities come only once

kwambox

Reommend me. Some work I do with my hands some I do with my …

reypatrp

Unajua hio ni shamba kiasi gani North Coast na unakataa waaah 🤣🤣🤣

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *