Museveni awazuia wafuasi wa People Power kwenye Twitter

Image result for museveni blocks followers

Rais Yoweri Kaguta Museveni atishika na kuanza kuwazuia wafuasi wa upinzani kwenye mtandao wa Twitter.

Museveni ambaye amekuwa miongoni mwa viongozi wenye wafuasi wengi kwenye mtandao anatazamiwa kupunguza chini ya milioni baada ya kuwakomesha watu wanaomkejeli na kudihaki uongozi wake. Museveni amekuwa kwenye ulingo wa utawala tangu mwaka wa 1986 hadi wa leo.

Mtazamio wa kupunguzika kwa wafuasi kwa Twitter umetokana na changamoto ambazo zimeletwa na ziara zake nchini Uganda ambazo wanasema siyo sahihi.

Museveni ‘amechoka’ kushinikizwa kwake na pia kuona heshtegi ambayo imekuwa maarafu wa #PeoplePower na #FreeStellaNyanzi na akawazuia.

Mwezi jana, museveni alimtoa msanii Jose Chameleone kwa orodha ya watu anaowafuata kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutoka chama chake tawala cha NRM na kujiunga na DP cha upinzani.

Hii iliashiriwa baada ya mwandishi mmoja wa Uganda kumwuliza mbona anafanya ziara sasa wakati amekuwa na muda wa miaka 30 kufanya hivo, na jibu lake lilikuwa kumng’oa jamaa huyo kutoweza kuona kazi zake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *