Willy Paul anaswa na kamera akitishia kutoa bunduki (Video)

Image result for willy paul threatens someone

Video ya msanii wa injili Willy Paul Msafii akitishia kutoa bunduki imesambaa kwenye mitandao.

Msanii huyo kupitia video iliyorekodiwa ameonekana akibishana na mwanaume mwingine juu ya nafasi ya maegesho katika moja ya majengo jijini.

Mwimbaji ambaye kamwe hataki kupuuzwa alithubutu kutoa bunduki yake kumaliza malumbano hayo ‘kama mwanaume’.

Image result for willy paul threatens someone

Imekuwa wiki moja tangu Willy paul akiri kupenda bunduki na kulingana na mtaalam wa usalama ambaye alishiriki maoni yake katika chapisho letu la mapema, ni kinyume ya sheria kuonyesha bunduki wazi kwa umma bila mavazi ya polisi.

Walakini, mwimbaji huyo mpenda kuvuma, anapenda kuweka vitu vyake wazi na hii ndio njia yake ya maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *