Kasaija ashindwa kati ya kufuata sheria ama kukiuka amri ya Museveni

Image result for kasaija

Waziri wa fedha Matia Kasaija yupo kwenye hali ya sintofahamu kutojua kama kufuata sheria ama kumtii rais Museveni kwenye uamuzi wa UTL ambapo atakuwa anakiuka sheria.

Bwana Kasaija amekwama kati ya kufanya ukaguzi wa UTL kama ilivyoagizwa na rais ama kufuata mwanasheria mkuu William Byahuranga ambaye alisema sio halali.

Rais Museveni alikuwa amemwagiza Evelyn Anite kukagua kampuni hiyo ya mawasiliano kufuatia ‘fununu’ alizozipata kuhusu wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Image result for uganda attorney general

Kabla Anite hajafanya Ukaguzi kw akampuni hiyo, mkubwa wake waziri Kasaija alimwandikia mwanasheria mkuu akiuliza wosia wake kuhusu hilo kulingana na sheria.

Mwanasheria Mkuu alisema kuwa UTL ambayo inasimamiwa na korti, itabidi ifanyiwe ukaguzi baada ya kipindi chao cha Novemba mwaka huu.

Mwanasheria Byahuranga alimwandikia waziri wa fedha akimwambia kuwa wizara haina mamlaka ya kufanya ukaguzi kwa kampuni yenyeinasimamiwa na serikali.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *