“Nilifunga virago mara tatu,” Mercy Masika aelezea changamoto kwenye ndoa

Image result for mercy masika and husband

Wanandoa wa nguvu wa Injili Mercy Masika na mumewe mchungaji David Muguro wameelezea hadithi yao ya upendo na jinsi walivyokutana.

Akiongea na Samantha Bridal, David alikumbuka siku alimpata Mercy Masika.

“Mara ya kwanza nilimwona Masika ni alipokuwa akiburudisha kwenye harusi moja nilipokuwa nikirekodi video. Alikuwa anaimba na nilitaka kumwambia aimbe kwenye harusi yangu, aimbe wimbo huo huo.”

Msanii huyo wa injili alipatia nambari ya simu bila kujua kuwa siku moja atakuwa mke wake.

“Nilikuwa mtu mzuri na ningewapatia nambri yangu kila mtu. Alikuwa ananitumia maandiko ya Bibilia mara kwa mara na sikumkumbuka maanake niliwapatia wengi.”

Mercy Masika and family

Baada ya miezi tano, Masika na David walipatana tena na hapo ndipo walipopendana.

David kwa wakati huo hakutaka kuonekana kwenye vyombo vya habari kwa hivyo akamsihi Masika kutomweka hadharani lakini haukufaulu.

“Wazazi wangu walikuwa wananisukuma kuolewa na wakaniambia ninafaa kuolewa baada ya kujua mtu kwa miezi sita ambayo walisema inatosha kujuana na kukaa kwa mda sio nzuri kwa desturi ya Wakristo,” Masika alielezea.

Wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka tisa sasa na ijapokuwa kuna mapenzi na riziki, Masika anasema kuwa ndoa yao haijakuwa laini bali kuna milima na mabonde kwa kila jambo.

Image result for mercy masika and husband

“Kuna siku nilikuwa nimefunga virago vyangu nikisema naenda kwetu nyumbani akakuja akaniongelesha tukaelewana. Hii ni ndoa na niliona kama kazi yangu ni kupika jikoni huku mume wangu anatazama televisheni kama mfalme, niliona kama nimeshindwa,”

Baada ya kuhudhuria mafunzo kadha wa kadha kuhusiana na ndoa, maisha yamebadilika kwa wanandoa hawa ambao wamebarikiwa na wana wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *