Diamond afichua habari zisizojulikana juu ya collabo yake na Akothee

Image result for akothee and diamond platnumz

Madam Boss Akothee silo jina geni kwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii. Akothee bila shaka ni mwanamke anayefanya kazi kwa bidii ambaye angefanya mengi kufanya nyimbo zake zichezwe.

Yeye na nyota wa bongo Diamond Platnumz alishirikiana kwenye wimbo wa Sweet Love miaka chache zilizopita, uliopokelewa vizuri kote Afrika Mashariki na mipakani.

Hadi wa leo, Akothee ndiye msanii wa kipekee wa Kenya aliyefanya collabo na Diamond. Mara tu baada ya collabo yao kufanyika, mashabiki walishinikiza kuwa alikuwa ammelipa Chibu Dangote maanake hakuwa msanii mkubwa wakati huo.

Image result for akothee and diamond platnumz

Akothee baada ya hiyo alishirikiana na msanii wa Nigeria Mr. Flavor kwenye collabo ya give it to me. Uvumi wakati huo ulikuwa ukisema kwamba alikuwa amemlipa msanii huyu pesa ile ile aliyolipa Diamond.

Alipoulizwa kama alimlipa shilingi milioni mbili za Kenya Diamond, Akothee alikiri kwa Eric Njoka kuwa;

“Milioni mbili ni nini? hiyo ni pesa ya njugu karanga. Siseme la au ndio lakini kama tulilipa na mziki haukuwa nzuri basi tungeitisha pesa zetu.”

Kituo kimoja humu nchini ilikaa na Diamond na kumuuliza uvumi huo ambapo alikiri kuwa hakulipwa ata kufanya collabo nae.

“Akothee hakunilipa kitu, nilifanya naye mziki kwa sababu ya ile nia na ari yake ya kufanya kazi kwa bidii,” Diamond alisema.

Hii ni collabo ya Diamond na Akothee;

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *