Orodha ya watu 10 mashuhuri wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao

Umewahi iuliza watu maarufu wenye ushawishi kwenye mtandao wanapata hela zao vipi? Washawishi ni baadhi ya watu wanaolipwa vizuri kwenye ulimwengu wa masoko.

Kupanda ngazi kwa mtandao wa kijamii inahitaji bidii na kujituma ili kupata kujulikana. Hata hivyo, kwa wengine, talanta yao inawavuta wafuasi bila kuhangaika.

Hawa ni baadhi ya wasanii na washawishi kwenye mtandao ambao wanalipwa mihela kochokocho.

  1. Akothee
  2. Image result for akothee weave

Madam Boss kwa kweli anasisimua wafuasi wake na ni miongoni mwa watu maarufu waliotajwa kuwa na ushawishi mkubwa nchini.

Kwa upande wa hela, anazo kama zote. Amejenga jumba kubwa na watoto wake wanasomea Ufaransa. Mama wa watano pia ni msanii na mwanabiashara kwenye kampuni yake ya Akothee safaris.

2. Njugush

Image result for njugush

Timothy Kimani almaarufu Njugush mekuja kupendwa na wengi kutoka televisheni hadi mtandao. Alionekana mara ya kwanza kwa kipindi cha Hapa Kule News na baadae The Real Househelps of kawangware.

Njugush amekuza talanta yake kwenye video za kuchekesha na kupata soko kubwa kutoka kwa makampuni iki ni pamoja na Safaricom.

Kwa sasa, Njugush anafanya ucheshi wake akiwa na mke wake, Celestine Ndinda.

3. Betty kyallo

Image result for Betty Kyallo

Mwanahabari Betty Kyallo sio mgeni kwa wengi maanake ameonekana kwenye televisheni mara kwa mara na kwa sasa yupo kwenye K24.

Mama wa mmoja ni miongoni mwa watu maarufu nchini na wafuasi wengi kwenye mtandao na biashara zake za nje kama Flair By Betty zimechangia kukuwa kwake kwenye ulimwengu wa mtandao.

4. Huddah Monroe

Image result for Huddah Monroe

Mwanamtindo Huddah anajulikana kwa urembo wake na kiuno cha nyigu kinachofanya wanaume kummezea mate kila uchao.

Hata hivyo, sio urembo tu aliobarikiwa nayo bali akili ya biashara kinachowafanya wanadada kumwonea wivu.

Kwenye ulingo wa mtandao, anatesa na mikosi zake za kufunga duka na ametajwa kuwa na ushawishi mkubwa.

5. Churchill

Image result for churchill ndambuki

Msanii na mcheshi Mwalimu Ndambuki amekuwa kwenye runinga kwa karibu miongo miwili sasa na anajulikana kwa kukuza talanta za wachesi kama Eric Omondi na wengine wengi.

Amekuwa pia na wafuasi wengi kwenye mtandao na ni miongoni mwa watu waliolipwa zaidi nchini kwenye sekta ya burudani.

6. Otile Brown

Image result for Otile brown

Msanii Otile na nyimbo zake za mapenzi amewavutia wengi na kiki baina yake na Vera Sidika pia kilichangia kumpa jina.

7. Kate Actress

Image result for kate actress kenya

Muigizaji Kate Actress ni miongoni mwa waigizaji ambao wameshikilia sekta ya uigizaji na kuipa maono tofauti na kukuza jamii.

8. Vera Sidika

Image result for Vera Sidika

Mrembo mwenye rangi nyingi Vera anajulikana kwa kuisimua wafuasi wake kwenye mtandao wa Instagram na kiungo chake cha mwili kilivyojibeba huwavutia wengi.

Vera pia ni mwanabiashara ambaye anatumia kiki kujipatia riziki na kwa kweli inamlipa.

9. Talia Oyando

Image result for Talia Oyando

Mtagazaji Talia Oyando amefahamika sana kupitia mziki wa raga na dancehall na amezuru nchi nyingi ikiwemo Jamaica ambayo ni nchi iliyobuni mziki huo.

Sauti yake nyororo na mapenzi yake kwa kazi yake imechangia kuwa na wafuasi wake.

10. Avril

Image result for avril kenya

Malkia wa Kenya Avril sio mgeni kwa wengi na talanta yake imempatia hela. Sote tunamjua Avril kwa nyimbo za miaka kumi zilizopita na bado anatesa.

Mwanamziki wa kike amekitunza kipaji chake na kubaki kileleni akiwatumbuiza mashabiki wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *