Duka kuu la Naivas lapigwa marufuku kwa kuuza nyama

Image result for meat section in naivas supermarket

Gavana wa Machakos Alfred Mutua siku ya Alhamisi alifunga sehemu ya nyama ya Naivas Supermarket katika kaunti yake.

Alifafanua kwamba hatua hiyo ilikuwa inahitajika kufuatia maelezo juu ya kemikali iliyowekwa ndani ya nyama.

Mwanahabari wa NTV, Dennis Okari alifichua siri hiyo ambayo soko ya nyama imekuwa ikitumia kulinda nyama kwa kutoharibika mapema.

Kemikali hizo ambazo zinawekwa kwa nyama kwa mujibu wa daktari, ni hatari kwa mwili na unaweza kusababisha saratani.

Gavana Mutua alisema kuwa baada ya kufichuliwa kwa siri hiyo, alichukua hatua ya kupima baadhi ya nyama zinazouzwa kwenye kaunti yake.

“Nimepewa ripoti ya maabara inayoonyesha kwamba sampuli ya nyama iliyouzwa kwenye Naivas Supermarket katika Gateway Mall katika Mavoko, kaunti ya Machakos, ilikuwa na miligramu 3,286 za ziada ambayo haipaswi kutumiwa kwa nyama,” inasoma ujumbe wa gavana.

Bw. Mutua aliongeza kuwa sehemu hizo za nyama zitasalia kufungwa hadi ukaguzi unapofanywa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *