Hizi ni baadhi ya nyimbo zimedondoka wiki hii

Ni Ijumaa murwa kabisa, na kama ibada, tunakuletea baadhi ya nyimbo ambazo zimedondoka juma hili na zinafanya vizuri kwenye YouTube.

Ni wakati wa kusahau wiki iliyo na shughuli nyingi na kuburudika wikendi inapoanza.

Haya ni baadhi ya nyimbo zilizotokea hii wiki;

  1. Vera Sidika – Mimi

Vera wiki hii aligonga vichwa vya habari baada ya kubadilisha rangi yake na kurudi jinsi alizaliwa, rangi ya mkaa.

Baadaye alidondosha ngoma mpya akitetea uhuru wa kutobagua rangi ya mtu na kuhamasisha umoja.

2. Lavalava+ Harmonize- Saula

Vijana wa Wasafi waamekuja na mdundo mkubwa kwa jina Saula. Wimbo huu wa Bongo unafanya vizuri na kutisha vilabuni hii wikendi.

3. Willy Paul+ Alaine- Shado Mado

Je, wakumbuka Shado Mado kati ya michezo tukiwa wadogo? Hii inamaanisha kuwa uache mafikra na ufurahie.

Baada ya kumlilie Alaine kwa kukata urafiki wao, Willy Paul amedondosha ngoma ya kibabe na malkia huyo wa Jamaica.

4. Tanasha Donna- Nah Easy

Mpenzi wa Diamond Platinumz hapendi mchezo roundi hii na licha ya kuwa mjamzito wa miezi saba, ana uwezo wa kufanya mziki na kutimisha malengo yake.

Nah Easy ndio jina la ngoma ya kidancehll na inashikilia nambari moja kwenye YouTube.

5. Rayvanny+ Rawlene- Girlfriend

Mbabe wa Bongo, Rayvanny amechnganya flow yake kwa kuimba Reggae akimshirikisha msanii wa Sauzi Rawlene.

Cheki kwenye Youtube ujionee jinsi kijana wa Wasafi anaweza kubadilisha mdundo na kushine kila kona.

6. Naiboi+ Ben Pol- Mmoja

Gwiji wa mziki wa Nairobi, Naiboi Worldwide pia amemshirikisha Ben Pol kwa wimbo wa mapenzi.

Naiboi alifanikisha collabo hii baada ya kufanya ziara Tanzania na viunga vyake pamoja na mahoiano kwenye vyombo vya habari.

7.  Wambui Katee- You

Malkia Wambui ambaye amekuwa akifanya remix za mziki ametoa wimbo wake wa pili baada ya kufana kwa Mahabuba.

Wambui pia anasherehekea maoni milioni moja kwenye Youtube.

Ametoa ‘You’ ambayo ni nzuri sana.

8. Ed-Sheeran-  No.6 collaborations project

Msanii wa Marekani Ed Sheeran ametoa albamu yake ya No.6 collaborations project ambayo amewashirikisha wasanii wengi wa mziki wa kufokafoka akiwemo Eminem, Stormzy, 50 Cent na Cardi B.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *