Moses Kuria awasuta Ruto na Raila

Image result for moses kuria

Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria amewahimiza Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kuacha mashambulizi ya kibinafsi dhidi yao.

Alisema tofauti kati ya viongozi wawili ni sababu ya kuongezeka kwa joto la kisiasa nchini.

“Kila siku katika habari ni kuhusu Ruto na Raila huku Wakenya wakiendelea kuteseka. Ni wakati sasa wa kusahau hao wawili, “alisema.

Image result for moses kuria

Mwakilishi huyo alisema wazi kwamba viwango vya umasikini nchini vimeongezeka kwa kasi lakini viongozi wanaendelea kubishana bila kutoa suluhisho kwa wananchi.

“Tuna miaka kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu ujao lakini Wakenya wanaamka kila siku na kupata siasa kutoka kwa viongozi wao badala ya maendeleo,” alionngezea.

Kuria na viongozi wengine chini ya mwavuli wa Team Wanjiku walikuwa kwenye ziara ya Gilgil.

Alisema kikundi chake kilijitolea kuunganisha jamii zote nchini na kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo wanakabiliana nazo.

Mbunge wa zamani wa Madaraka, Reuben Ndolo alisisitiza ajenda ya maendeleo ya Rais Uhuru Kenyatta akibainisha kwamba siasa mbaya ulikuwa unaathiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *