Mtetezi wa wanawake na mwalimu Stella Nyanzi ametiwa mbaroni juu ya kuchora sehemu ya siri na kuitwika kwenye mtandao wa Facebook mwezi Septemba.
Mtetezi huyo katika shairi, alitumia maelezo ya wazi ya kuzaliwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, na uke wa mama yake kuashiria “unyanyasaji na ukandamizaji” wake nchini.
Stella ambaye alikuwa amesimama mbele ya Mahakama ya Barabara ya Buganda, alishtakiwa kwa “unyanyasaji na kutumia mtandao vibaya”.
Alishtakiwa kuwa na nia ya kuleta fujo na siri ya Rais, Yoweri Kaguta Museveni na mama yake marehemu Esteeri.
Shairi aliloliandika linasema;
Yoweri, walisema jana ilikuwa siku ya kheri ya kuzaliwa kwako.
Ni siku ya huzuni!Natumai sehemu ya siri yenye inanuka ingekukuacha umefariki.
Ikubanie kama unavyotubania na unyanyasaji na ukandamizaji.
Yoweri, nasikia jana ilikuwa siku ya kheri ya kuzaliwa kwako,
ni siku ya huzuni.