Njugush matatani baada ya kushindwa kulipa hotelini akijaribu kumfurahisha mpenzi wake wa zamani

Mwigizaji na mcheshi Blessed Njugush huwa na mikosi akiwa na mke wake Celestine Ndinda almaarufu Wakavinye na yanaonekana kumzidia.

Njugush alijipata matatani baada ya kushindwa kulipa bili ya hoteli.

Mcheshi huyo aliend hotelini na kwa bahati mbaya au nzuri, akapatana na mchumba wake wa zamani humo humo akijipakulia chamcha.

Baada ya kuona hivo, Njugush akaamrisha aletewe chakula cha bei ghali ili kumuabisha mchumba wake wa zamani kwamba ana hela si haba.

“Waiter, nataka samaki na nyama fry, kinywaji ni kile cha kawaida cha elfu nane,” alimwashiria mhudumu.

 

Alipoulizwa mbona anapiga mayowe akiongea akajibu, “nataka huyu msichana hapo kando asikie anachokikosa kwenye maisha yake kwa sababu ni mchumba wangu wa zamani.”

Baada ya Njugush kumaliza mapochopocho, ilifika wakati wa kulipia na alipigwa na butwaa alipojua kuwa pesa zake zilitokomea njiani alipokuwa akielekea kwenye hoteli.

Mchumba wake wa zamani alipasuka kwa kicheko na kumwambia kuwa alimwacha kwa sababu hana pesa na ndivyo hali ilivyo kwenye hoteli hiyo.

Njugush alishindwa kujitetea kwa namna yoyote ile kwa vile mfukoni hakuwa na ‘any’.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *