Dennis Itumbi kusalia kituo cha polisi cha Muthaiga kwa siku 5

Image result for dennis itumbi charged in court

Mtaalamu wa kidigitali Dennis Itumbi atabaki siku tano kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga kama wapelelezi wanachunguza jinsi alivyohusishwa na barua ya mauaji ya bandia dhidi ya Naibu Rais William Ruto.

Itumbi alikuwa mbele ya jaji wa mahakama ya Milimani Zainab Abdul huku uchunguzi ulitaka kumtia mbaroni kwa siku kumi na nne ili kusaidia upelelezi mwafaka.

Zainab alisema kuwa siku 14 zilikuwa nyingi mno na simu ya Itumbi inafanyiwa uchunguzi.

Image result for milimani court

Itumbi alikuwa amepinga kufungwa, akitetea kuhusu usalama wake. Aliomba kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani ama kutiwa mbaroni kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga, Gigiri au Kileleshwa kama hangepewa dhamana.

Alisema kuwa kituo cha polisi cha Kamukunji ambayo iliorodheshwa haiko salama.

Itumbi atasalia mbaroni hadi Julai 10 ambapo kesi yake itatajwa.

Alikamatwa Jumatano kwenye katikati mwa jiji la Nairobi juu ya barua bandia iliyoshinikiza mauaji ya naibu rais William Ruto.

Related image

Simu ya mkononi ya Dennis Itumbi ilichukuliwa na uchunguzi kufuatiliwa hadi ujumbe kupitia Whatsapp ambapo kuna kikundi cha Tangatanga ambacho ina watu zaidi ya 256.

Kwa kujitetea, upande wa Itumbi ulisema kuwa mshukiwa hana semi lolote kwa kikundi hicho ambacho kina magavana, wabunge na wanachama wa Tangatanga na hamna haja ya kushika mtu ambaye sio maarufu kwa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *