Baadhi ya watu mashuhuri ambao wamefariki mwaka 2019

Image result for funeral in kenya

Wakenya wamepitia changamoto kwenye nusu ya mwaka ambayo ilikamilika siku ya Jumatatu na imesalia siku 183 kabla ya mwaka kuisha.

Ilianza vibaya kwenye uchumi baada ya kupitia uchaguzi mkuu na mvua ambayo ilipotea kwa miezi mitatu mtawalia.

Image result for drought in kenya

Pia kwenye miezi sita, Kenya imepoteza vigogo wakubwa kwenye ngazi za juu humu nchini kutoka kwa wasanii, wanasiasa na wakurugenzi.

Hawa ni baadhi ya watu mashuhuri waliotuacha kwa muda huo mwaka huu;

  1. James Oduor (Cobra)

Image result for james oduor cobra

Mchezaji James Oduor almaarufu Cobra aliaga dunia baada ya shabulizi la kigaidi kwenye hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi.

Alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye hoteli hilo akingojea kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake.

2. Chris Kantai

Image result for chris kantai

Rapa shupavu tena Mkongwe Chris Kantai alituacha baada ya kuroipotiwa kufariki juu ya ulevi.

Kantai alikuwa na uraibu wa ulevi na baada ya kupelekwa kwa vyumba vya kurekebisha tabia ambapo alitoa uraibu wake lakini baadae akarudi tena.

Japo rapa Khaligraph Jones alijaribu kumleta mkongwe huyu kwa mziki, lakini vyombo vya habari havikumpatia chanzo kikubwa cha kujiokoa kwenye mziki na kubakia kurudi ulevini.

3. Kone Nouhoum

Image result for Kone Nouhoum

Huyu ni mwigizaji mashuhuri na alipata ajali mwaka jana kwenye sehemu ya Geothermal na amekuwa akipigania uhai wake.

Kifo chake kilikuwa pigo kwa sekta ya uigizaji Kenya.

4. Jonathan Moi

Image result for Jonathan Moi

Mwana wa kwanza wa rais mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi ambaye alikuwa ni dereva wa magari za Safari Rally na alifariki kwenye siku ya Pasaka.

5.  Bob Collymore

Image result for bob collymore

Hii ilikuwa pigo sana kwa Wakenya na iliwashangaza kwa kifo cha ghafla. Bob Colymore alikuwa mkurugenzi mtendaji wa Safaricom. Bob aliwakuza wengi kwenye sekta ya usanii na ufundi ambacho waliofaidika na wafuasi wa kampuni ya Safaricom wamekiri.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *