Jenerali Sejusa ampa Bobi Wine ushauri jinsi ya kumshinda Museveni uchaguzi wa 2021

Image result for general david sejusa message to bobi wine

Mratibu wa zamani jeshi David Sejusa almaarufu Tinyefunza amemwambia Bobi Wine hatomshinda rais Yoweri Kaguta Museveni kwenye uchaguzi ujao wa mwaka wa 2021.

Jenerali Sejusa ambaye alipaswa kustaafu mwaka huu alipata jina lake limetolewa kwenye kundi la watu wa kustaafu kwenye jeshi.

Jenerali huyo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kumng’atua Museveni na kuongezea kuwa uchaguzi haitawahi kumtoa mamlakani.

Image result for general david sejusa message to bobi wine

“Naona wengi wenu wanangoja 2021 ndio wamtoe Museveni, ningetaka kuwaambia hakuna tofauti itafanyika,” alisema Sejusa.

“Museveni ameshindwa mara tatu kwa uchaguzi tatu zilizopita na bado yuko afisini, kama mnataka kumtoa mamlakani msahau mambo na uchaguzi,” aliongezea.

Sejusa alisisitiza kuwa viongozi kama hao wanapaswa kutolewa kwa namna vyovyote vile ata kutumia bunduki.

Image result for museveni

Alimshauri Bobi Wine kwamba asahau mambo na kutoa wito kwa watu kuchukua itmbulisho akisema kuwa Museveni ndio wa kuzichapisha vitambulisho hivyo na havitasaidia kushinda uchaguzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *