Lilian Muli amtakia mema mpenzi wake wa zamani

Image result for lilian muli and kanene

Mtangazaji mashuhuri Lilian Muli amemtakia mwenziwe Moses Kanene maisha nzuri kwa uhusiano na mpenzi wake mpya.

Lilian Muli aliachana na baba wa mtoto wake miaka saba iliyopita na sasa wote wamepata wachumba.

Image result for lilian muli and kanene

Hii ni baada ya picha za Kanene na mpenzi wake mpya kusambazwa kwenye mitandao hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Word Is, kwenye mahojiano ya kipekee na Lilian Muli, alisema kuwa hana kinyongo na mpenzi wake wa zamani kwani wote wamepiga hatua na wana furaha.

“Wanaonekana wenye furaha pamoja, na sina chochote cha kusema. Tumetengana kwa miaka saba na nina mchumba wa kwangu, mbona nimnyime furaha wakati nina furaha kwangu? Yote ni sawa,” alisema Muli.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Kanene amekuwa akimchumbia meneja wa benki kwa mda sasa na ni mjane wa watoto wawili.

Moses Kanene with his new catch Grace Nungari
Kanene na mpenzi wake mpya

Kwa kumbukumbu tu, Lilian Muli na Kanene walifunga pingu za maisha mnamo 2009 pale Windsor Golf. Waliachana mwaka wa 2016 baada ya Muli kuadika ripoti juu ya udanganyifu wa bwana wake na kuenda nje ya ndoa.

Wawili hao wana mtoto mmoja mvulana na bado wanamlea pamoja.

Image result for lilian muli and kanene

Muli aliwasilisha talaka tarehe 7 Januari 2016, katika Mahakama kuu Milimani, Nairobi. Alitoa udanganyifu na ukatili kwenye ndoa.

Muli alisema aliugua ugonjwa wa akili kwa sababu ya maisha ya kashfa mumewe alimwongoza na ukatili wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *